Rais Kenyatta : Washenzi Wanikome!

Rais Uhuru Kenyatta amewasuta baadhi ya viongozi haswa kutoka eneo la kati wanaodai hajaleta maendeleo katika eneo hilo na badala yake kuyaelekeza kwingine,na kuwataja kama washenzi.
Kenyatta anasema lengo lake ni kuwahudumia waKenya wote na kwamba siasa kama hizo ni duni na zimepitwa na wakati.
Rais alikuwa akizungumza Pwani ya Kenya katika bustani ya Mama Ngina Drive ambako alizindua ukarabati wa bustani hiyo kwa gharama ya shilingi Milioni mia nne sitini kwa lengo la kuvutia watalii zaidi.