Mauaji Kiambu : Video yafichua yaliyojiri kabla mke kuuawa

K24 imebaini kuwa uhusiano wa kindoa wa mwendazake Mary Wambui Kamangara na mumewe Kori Karuwe uliashiria misukosuko iliyosheheni ugomvi na migogoro.
Hata wakati fulani kukiwa na majibizano makali kati ya wanandoa hawa yaliyoonekana kuhatarisha maisha ya Kori Karuwe na mkewe Mary Wambui.
Aidha K24 imeweza kupata nakala ya video ambayo inadaiwa kurekodiwa nyakati za mwisho mwisho na mwendazake, ambapo wambui alikuwa mwingi wa masimango na hofu kuu.