Historia ya Diamond yawatoa machozi Tandale/ aeleza alivyotoswa mpaka kufanikiwa

Msanii wa WCB Diamond Platnumz, Ijumaa hii ametoa misaada mbali mbali kwa wakazi wa eneo la Tandale ambapo amezaliwa na kukulia. Muimbaji huyo ametoa bima kwa wakazi wa eneo hilo, boda boda kwa vijana, fedha za miradi lakini kubwa zaidi ni historia ya maisha yake aliyoitoa yenye kusikitisha na kukutoa machozi.